Haki na Majukumu ya Mhusika kwa Swahili

Mswada wa Haki na Majukumu ya Mhusika uliandikwa kwa mara ya kwanza kwa Kiingereza mwaka wa 2003. Ulipitiwa tena mwaka wa 2007. Umetafsiriwa kwa lugha mbalimbali, kama ilivyoorodheshwa hapa chini. Ukiamua kuhusika katika uchunguzi wa Mtandao wa Majaribio ya Chanjo ya HIV (HVTN), utapewa nakala ya hati hii kwa lugha moja kati ya lugha hizi, kulingana na mapendeleo yako. Huenda maneno ya hati ambayo unapokea yawe tofauti kidogo na maneno yalliyo hapa chini.

The Participants' Bill of Rights and Responbilities are available in the following languages:
Afrikaans | Bemba | ChichewaEnglish | Nyanja | SepediSetswana | ShonaSotho | Spanish | TsongaXhosa | Zulu | French | Portuguese

Haki

Kama mhusika katika utafiti wa MMCH, una haki ya:

 • Kupokea maelezo yote yanayojulikana, ikiwa ni pamoja na hatari na faida zinazoweza kutokea ukihusika katika uchunguzi, ulizowasilishwa kwa njia unayoweza kuelewa. Utaelezwa kuhusu habari yoyote mpya uliyojifunza katika utafiti huu.
 • Kukataa kushiriki katika utafiti huu au kuamua kuuwacha wakati wowote. Unaweza pia kukataa kushiriki katika utafiti wowote wa ufuatiliaji utakaoalikwa kushiriki. Hutapoteza haki zozote zinazorejelewa katika hati hii iwapo utakataa kujiunga na utafiti au kuuwacha.
 • Mazingira ya utafiti yasiyokuwa na ubaguzi. Chaguo za kibinafsi, maadili, imani na muktadha wa kitamaduni utaheshimiwa na watu wanaofanyautafiti huu.
 • Kupelekwa rufaa kwa huduma zinazopatikana za ushauri na usaidizi kwa maswala yanayohusiana na utafiti na uzuiaji virusi vya HIV.
 • Kupelekwa rufaa kwa huduma zinazopatikana za ushauri, usaidizi, dawa, na tiba ya magonjwa unayougua wakati wa utafiti, ikiwa ni pamoja na HIV.
 • Usaidizi katika kutatua matatizo na/au ubaguzi wa kijamii unaohusiana na utafiti huu. Ukituruhusu, tunaweza kuzungumza na watu unaotuomba tuwasiliane nao ili tufafanue kuhusu kushiriki kwako katika utafiti.
 • Matibabu ya majeraha ya kimwili, iwapo yatatokea, kwa jeraha lolote linaloweza kuhusiana zaidi na bidhaa au utaratibu wa utafiti huu kuliko kisababishi chochote kingine kile, kama ilivyoelezwa katika fomu ya idhini ya utafiti. Kuna fedha za kulipia matibabu ya majeraha haya. Kikundi kinachohakiki maswala ya usalama ya utafiti huamuza kuhusu uhusiano wa jeraha na utafiti huu. Unaweza kukata rufaa ikiwa hukubaliani na uamuzi. Katika hali nyingine, huenda fedha hizo zisitoshe kushughulikia matibabu yote. Vikundi vinavyohusika katika utafiti vitatafuta fedha zaidi ikihitajika, lakini haviwezi kukuahidi kwa uhakika. Wahudumu wako wa utafiti watatoa maelezo zaidi kuhusu swala hili na watajibu maswali yoyote ambayo huenda umeyawasilisha au kukupa rufaa kwa mtu aliyehitimu kabisa kujibu maswali yako.
 • Kipimo kisicho na malipo na sahihi cha maambukizo ya HIV wakati wa utafiti. Ikiwa, mwishoni mwa utafiti huu, kipimo kinaonyesha una HIV iliyosababishwa na chanjo ya utafiti na wala si maambukizo ya HIV, unaweza kupokea kipimo cha ufuatiliaji katika kliniki ya utafiti hadi kipimo kionyeshe huna HIV.
 • Usaidizi katika kufikia ahadi za utafiti. Orodha ya vifaa utakavyopewa itatolewa na kituo chako cha utafiti.
 • Faragha. Mawasiliano na maelezo yako na ushiriki wako katika utafiti utasambazwa kama inavyohitajika ili kutekeleza utafiti, au inavyohitajika na sheria. Tazama fomu yako ya ridhaa ya utafiti kwa maelezo zaidi.
 • Kupewa kadi ya utambulisho wa utafiti inayoonyesha kwamba unahusika katika utafiti. Kadi hii ya hiari itajumuisha nambari ya simu na/au anwani ya mtu anayeweza kutoa maelezo zaidi.
 • Kudumisha haki zako za kisheria. Kama mshiriki wa jaribio, hakuna haki yako yoyote unayoondoa.
 • Kufahamishwa kama ulipokea kipozaungoau chanjo utafiti ukikamilika, au ikihitajika kimatibabu.
 • Kuelezwa kuhusu utafiti unavyoendelea, kufahamishwa wakati matokeo ya utafiti yanaweza kupatikana, na kuambiwa jinsi ya kupata matokeo.

Majukumu

Kama mshiriki katika utafiti wa MMCH, una jukumu la:

 • Kuhakiki na kuonyesha kuwa unafahamu vifaa vyote ulivyopewa, ikiwa ni pamoja na hati za ridhaa. Kuuliza ufafanuzi kuhusu maelezo yoyote usiyoyaelewa kabla ukubali kuhusika katika utafiti. Unaweza pia kuuliza maswali wakati wowote wakati wa utafiti.
 • Kufanya uamuzi wa ridhaa kuhusu iwapo utahusika katika utafiti baada ya kuzingatia kuhusu hatari na faida. Ni muhimu ujue maudhui ya utafiti . Wahudumu watakusaidia kuhusu swala hili. Zungumza na watu unaowaamini na kuwaheshimu kuhusu ikiwa inafaa ushiriki katika utafiti, ikiwa kuzungumza nao kutakusaidia kufanya uamuzi wa busara
 • Wafahamishe wahudumu wa utafiti haraka iwezekanavyo ikiwa utabaguliwa/au kuathiriwa kijamii , hali amabayo unaamini inahusiana na kuhusika kwako katika jaribio hili.
 • Usitoe damu au kungo ch amwili au viowevu vyovyote vya mwili wakati huu wa utafiti.
 • Pimwa virusi vya HIV katika eneo la utafiti katikakipindi chote cha utafiti. Zungumza na wahudumu wa utafiti ikiwa unalazimika kupimwa mahali pengine
 • Ikiwa una uwezo wa kuwa mjamzito, epuka ujauzito wakati wa utafiti kwa kutumai mbinu za kupanga uzazi. Wahudumu watakusaidia kuhakiki mbinu mwafaka za kupanga uzazi .
 • Zingatia miadi yako ya utafiti. Wafahamishe wahudumu haraka iwezekanavyo ikiwa unahitaji kupanga miadi upya.
 • Waheshimu wahudumu.
 • Weka siri kuhusu kuhusika kwa watu wengine katika utafiti.
 • Wape wahudumu wa utafiti maelezo kamili na sahihi yanayohusiana na utafiti. Wafahamishe wahudumu wa utafiti ikiwa kuna mabadiliko yoyote katika maelezo yako ya mawasiliano au afya.
 • Fuata maagizo ya wahudumu wa utafiti kadri ya uwezo wako. Shirikiana na wahudumu wa utafiti ili kudumisha afya na usalama wako wakati wa jaribio.
 • Wafahamishe wahudumu wa utafiti haraka iwezekanavyo ikiwa huwezi kuendelea au ikiwa utaamua kuwacha kuhusika katika utafiti.